Saturday, 10 September 2011

Feri yazama Zanzibar


Idadi kubwa ya watu inahofiwa imepoteza maisha kufuatia kuzama kwa meli iitwayo MV Spice ilokuwa ikitoka Unguja kwenda Pemba. Ajali hiyo ilitokea katika mkondo wa Nungwi unaojulikana kwa maji makali mwendo wa saa saba usiku wa kuamkia leo.

Msajili wa meli wa zanzibar amesema meli hiyo ilikuwa na leseni ya kubeba abiria 600 lakini wasi wasi umekuwa mkubwa kwa vile meli za Unguja na Pemba hujaza bila kiasi.

Mpaka sasa watu wasiopungua 163 wamekufa, aidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo, lakini watu 325 walionusurika wameokolewa, kwa mujibu wa waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar.

Shughuli ya uokoaji inaendelea hivi sasa na tayari serikali ya Zanzibar imeanza mipango ya kupokea  maiti 

Source: BBC Swahili 

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

ni msiba mkubwa poleni wafiwa wote na wajerehiwa wote. mwenyezi mung awape nguvu kwa kipindi hiki kigumu.